Tuesday, October 30, 2012

Mpeni ale chakula,asije kutuibia
Awe amevimba sura,awe kama katupia
Tena mwenye mkarara,ule uliokimbia
Hapendi kurudi kwao,kisa wamemtukana
 
Kisa wamemtukana,hapendi kurudi kwao
Ameanzisha zahama,za kujipiga matao
tena hapaoni nyuma,kule kwa kina Mkao
Hapendi kurudi kwao,kisa wamemtukana
 
Hana dharimu hukumu,huyu mama wa makamo
Tena wetu wa muhimu,yule mwenye msimamo
Hajui kumwaga damu,hata kwa kulima ngano
Hapendi kurudi kwao kisa wamemtukana

heee! heee! heeeee!!! Pata uhondo mwana kwetu ni burudani kwa kila aina ya kina Tafakari,Fikiri halafu ona kile usichokijua

haya sasa kila kitu kwa kila mtu... hapa sijui nini ahaa jamani maisha kweli ni zaidi ya vile tunavyofikiri na kuona haya bwana

No comments:

Post a Comment