Tuesday, October 30, 2012

BADO SIKU KADHAA

Malezi youth theatre,ina kila sababu ya kujivunia kuwa kampuni sanaa inayojiendesha kwa mfumo wa kusaidia jamii. Kampuni hii inatumia nguvu nyingi katika kutenda kazi zake ili kuhakikisha jamii ya watanzania inapata kile ambocho ilikuwa inakikosa kwa muda mrefu.Tunjua kuwa maisha ni kila kitu lakini kuna vitu vingine sio maisha hebu tujipange na tuweke mambo hayo katika hali hiyo. Tuifanye jamii kuwa katika hali ya kufurahi na kupunguza misono ya mawazo kwa mfano
  1. Kuandaa sanaa yenye kumfikirisha na kumfurahisha kwa wakati huo huo kuchukua hatua ya kujikomboa na misongo
  2. kuifanya jamii iwe na furaha wakati wote
  3. kuwajengea uwezo wa kujiamini vijana wetu katika mashindano ya kiuchumi na kijamii
  4. kuuweka utamaduni wetu katika nafasi ya juu kidunia ili kila mtanzania aweze kujivunia
hivyo ili kuwafanya wanajamii kuwa katika hali ya kufanya maamuzi Malezi itahakikisha inatumia ujuzi wa kisanaa kuwapa watanzania kile kinachostahili

No comments:

Post a Comment