Tuesday, October 30, 2012

Mpeni ale chakula,asije kutuibia
Awe amevimba sura,awe kama katupia
Tena mwenye mkarara,ule uliokimbia
Hapendi kurudi kwao,kisa wamemtukana
 
Kisa wamemtukana,hapendi kurudi kwao
Ameanzisha zahama,za kujipiga matao
tena hapaoni nyuma,kule kwa kina Mkao
Hapendi kurudi kwao,kisa wamemtukana
 
Hana dharimu hukumu,huyu mama wa makamo
Tena wetu wa muhimu,yule mwenye msimamo
Hajui kumwaga damu,hata kwa kulima ngano
Hapendi kurudi kwao kisa wamemtukana

heee! heee! heeeee!!! Pata uhondo mwana kwetu ni burudani kwa kila aina ya kina Tafakari,Fikiri halafu ona kile usichokijua

haya sasa kila kitu kwa kila mtu... hapa sijui nini ahaa jamani maisha kweli ni zaidi ya vile tunavyofikiri na kuona haya bwana

UKIONA KUNA JAMBO....

Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa utamaduni. Katika kuhakikisha Tanzania inakuwa mbele kwenye utamaduni, ni lazima tuhakikishe kuwa kila kijana anajipanga kiuhakika kabisa kwenye maisha. Leo tunaona muingiliano wa kijamii,kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni wenyewe wanauita utandawazi lakini je sisi kama watanzania tumejipangaje?

Ole wenu nyinyi mliobeba mizigo ya nguo halafu makombe maji... Na ole wako wewe uliobeba jiwe halafu ukautamani mkate. Na ya nini kubeba mizigo isiokuwa na faida? Dunia ni yetu Malezi youth theatre ipo tayari kuiuhisha jamii ya Tanzania kwa kuhakikisha kila nukta ya uatajiri wake wa kiutamaduni unatumika katika kumuweke kifua mbele kijana wa Tanzania.

Leo ndio hivyo ukiona kuna JAMBO ujue lazima nyuma kitakuja KIJAMBO je tupo tayarii


Hapa ni nyumbani kwetu. Mungu ametuumba ili tuje tupatumie. Je tangu umezaliwa umeshatumia asimia ngapi ya ya vile unavyoviona? Unaitumiaje akili yako kutumia hivyo unavyoviona? MALEZI YOUTH THEATRE ipo kwa ajili hiyo tuataitumia tu. Utajiri wetu umaskini sio wetu kwa sababu huwa haumpi mtu furaha hivyo lazima tuupige vita

BADO SIKU KADHAA

Malezi youth theatre,ina kila sababu ya kujivunia kuwa kampuni sanaa inayojiendesha kwa mfumo wa kusaidia jamii. Kampuni hii inatumia nguvu nyingi katika kutenda kazi zake ili kuhakikisha jamii ya watanzania inapata kile ambocho ilikuwa inakikosa kwa muda mrefu.Tunjua kuwa maisha ni kila kitu lakini kuna vitu vingine sio maisha hebu tujipange na tuweke mambo hayo katika hali hiyo. Tuifanye jamii kuwa katika hali ya kufurahi na kupunguza misono ya mawazo kwa mfano
  1. Kuandaa sanaa yenye kumfikirisha na kumfurahisha kwa wakati huo huo kuchukua hatua ya kujikomboa na misongo
  2. kuifanya jamii iwe na furaha wakati wote
  3. kuwajengea uwezo wa kujiamini vijana wetu katika mashindano ya kiuchumi na kijamii
  4. kuuweka utamaduni wetu katika nafasi ya juu kidunia ili kila mtanzania aweze kujivunia
hivyo ili kuwafanya wanajamii kuwa katika hali ya kufanya maamuzi Malezi itahakikisha inatumia ujuzi wa kisanaa kuwapa watanzania kile kinachostahili